Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili aachilie nguvu za Mungu katika injili

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Unleash the Power of God in the Gospel

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 43 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni
upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu”
(1 Wakorintho 1:18)

“Mimi siionei haya Injili ya Kristo kwa maana ni uweza wa
Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwanza kwa Myahudi
na kwa Myunani pia” (Warumi 1:16)

Neno “injili” linamaanisha habari njema. Wakati tunapohubiri injili tunatangaza habari ambazo zinawaletea watu furaha kwa sababu ni habari njema. Injili ni habari njema kwa sababu kweli itawafanya watu wawe na furaha ya milele.

Ujumbe wa injili ni kifo na kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo. Mtume Paulo anasema jambo hili wazi wakati anasema, “Basi ndugu zangu nataka niwakumbushe kuhusu Injili niliyowahubiria, mkaipokea na ambayo katika hiyo mmesimama. Kwa Injili hii mnayookolewa mkishikilia kwa uthabiti neno nililowahubiria ninyi. La sivyo, mmeamini katika ubatili. Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemayo Maandiko, ya kuwa alizikwa na alifufuka siku ya tatu, na kwamba alimtokea Kefa, kisha akawatokea wale kumi na wawili. Baadaye akawatokea wale ndugu waamini zaidi ya 500 kwa pamoja, ambao wengi wao bado wako hai, ingawa wengi wamelala. Ndipo akamtokea Yakobo na kisha mitume wote.” (1 Wakorintho 15:1-7).

Ujumbe wa injili ni huu: Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, alizikwa, alifufuliwa na aliwatokea zaidi ya watu mia tano. Kwa hivyo ujumbe wa injili unahusu mambo ambayo yalitokea. Ujumbe huu hauhusu mawazo ya watu au hisia za watu, unahusu mambo ya ukweli ambayo yalitokea: kuzikwa na kufufuliwa kwa Kristo Yesu.

Kwa watu wengi ulimwenguni, ujumbe wa injili ni upumbavu kwao. Biblia inasema kwamba, “Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu” (1 Wakorintho 1:18). Hizi ndizo nguvu ambazo Kristo wakati alikufa aliachilia katika injili.

“Mimi siionei haya Injili ya Kristo kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwanza kwa Myahudi na kwa Myunani pia.” (Warumi 1:16).

Ni kwa nini kifo cha Bwana Yesu Kristo ni habari njema kwa wengi na ni upuzi kwa wengine? Kwa nini watu wengine hawamwamini Kristo ili waokolewe? Jibu la maswali haya limepeanwa katika Biblia: “Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu.” (2 Wakorintho 4:4). Kuongezea kwa haya ni kwamba mwanadamu amekufa katika dhambi zake na hawezi kuelewa ukweli ambao unatoka kwa Mungu. “Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kupokea mambo yatokayo kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa jinsi ya rohoni.” (1 Wakorintho 2:14).

Kabla ya mtu yeyote kuokolewa, macho yake lazima yafunguliwe na apewe uhai wa kiroho. Hii ndiyo sababu Biblia inasema, “Lakini kwa wale ambao Mungu amewaita, yaani, Wayahudi na Wayunani, Kristo ni nguvu na hekima ya Mungu” (1 Wakorintho 1:24). Sisi sote wakati moja tulikuwa tumepofushwa na shetani na tulikuwa tumekufa katika dhambi zetu. Lakini Mungu aliondoa upofu wetu na akatufanya kuwa hai kiroho. Hivi ndivyo tulivyookolewa. Ikiwa hujaokoka, basi wewe umepofushwa na shetani na umekufa katika dhambi zako. Mwombe Mungu akuondolee upofu wako na akufanye kuwa hai katika Kristo.