Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili amalize kutii sheria ili watu wake wawe wenye haki

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Complete the Obedience That Becomes Our Righteousness

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 11 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Akiwa na umbo la wanadamu, alijinyenyekeza hata mauti,
naam, mauti ya msalaba” (Wafilipi 2:8).

“Kwa maana, kama vile kwakutotii yule mtu mmoja, wengi
walifanywa wenye dhambi, vivyo hivyo, kwa kutii kwa mtu
mmoja, wengi watafanywa wenye haki”
(Warumi 5:19).

“Mungu alimfanya Yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa
ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu katika Yeye”
(2 Wakorintho 5:21).

“Nionekane mbele Zake nisiwe na haki yangu mwenyewe
ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani katika
Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu kwa njia ya imani”
(Wafilipi 3:9).

Wakati Mungu anamwokoa mtu anafanya mambo mawili. Kwanza anaondoa dhambi za mtu huyu. Pili anampatia mtu huyu haki ambayo inatokana na Kristo. Hii ndiyo sababu tunaweza kusema, “Nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani katika Kristo” (Wafilipi 3:9).

Tunapewa haki itokanayo na Kristo. Hii inamaanisha kwamba Bwana Yesu Kristo alitii sheria ya Mungu kikamilifu. Kwa hivyo wakati tunamwamini, anatupatia utiifu wake. Kwa njia hii tunahesabiwa wenye haki. Wakati Mungu anatutazama, haoni hesabu yetu ya dhambi, bali anaona haki ambayo hutokana na Kristo Yesu.

Hivi ndivyo Mungu anavyomhesabu haki mwenye dhambi (Warumi 4:5). Kwanza kabisa kifo cha Kristo kililipia dhambi zetu halafu tunapewa utiifu wake Kristo Yesu na katika mahakama ya Mungu tunahesabiwa wenye haki. Hivi ndivyo tunavyohesabiwa haki.

Mateso na kifo cha Bwana Yesu Kristo ndiyo msingi wa wokovu wetu. “Alijeruhiwa kwa makosa yetu” (Isaya 53:5). Kifo chake msalabani kilikuwa kitendo cha utiifu kwa Mungu Baba. Katika maisha yake yote alimtii Babake na kwa kifo chake alikamilisha utiifu wake: “Alijinyenyekeza hata mauti, naam, mauti ya msalaba (Wafilipi 2:8). Kwa sababu alitii, tutaingia mbinguni. “Kwa kutii kwa mtu mmoja, wengi watafanywa wenye haki” (Warumi 5:19).

Kwa hivyo ni kifo na mateso ya Kristo ndiyo msingi wa wokovu wetu. “Mungu alimfanya Yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu katika Yeye” (2 Wakorintho 5:21). Wakati Biblia inasema kwamba alifanyika dhambi kwa ajili yetu, inamaanisha kwamba dhambi zetu ziliwekwa juu yake na tumesamehewa kwa sababu alikufa kwa ajili yetu. Papo hapo tulipewa haki yake ili tuwe wenye haki machoni pa Mungu.

Kwa hivyo ndani ya Yesu kuna wokovu kamili: yaani dhambi zetu zimeondolewa na tumepewa haki yake. Haya yote tunayapokea kwa imani.