Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili aondoe hukumu yetu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Take Away Our Condemnation

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 12 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Ni nani basi atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye
aliyekufa; naam, zaidi ya hayo, ndiye aliyefufuka katika wafu,
yuko mkono wa kuume wa Mungu; naye ndiye anayetuombea”
(Warumi 8:34).

Kwa sababu Bwana Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya watu wake, Biblia hivi ndivyo inazungumza kuhusu wale ambao wameokoka: “Sasa, hakuna hukumu ya adhabu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu” (Warumi 8:1). Kuokoka inamaanisha kuwa katika ushirika na Kristo Yesu kwa imani. Wakati tunaokolewa tunaungana na Kristo Yesu. Tunaungana naye katika mateso na kifo chake, na kifo chake kinakuwa wokovu wetu.

Hii inamaanisha kwamba njia moja tu tunaweza kuokolewa, ni kwa imani ndani ya Kristo Yesu. Imani inatuleta kwa Kristo Yesu na haki yake inakuwa yetu. Mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ndani ya Kristo Yesu. Sisi tulimwamini Kristo Yesu ndipo tukahesabiwa mwenye haki na wala si kwa matendo ya sheria; “Mtu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria bali kwa njia ya imani katika Yesu Kristo” (Wagalatia 2:16). “Kuhesabiwa haki kwa imani” na “kuhesabiwa haki katikaKristo” (Wagalatia 2:17), yote mawili yanamaanishi kitu kimoja. Tuko ndani ya Kristo kwa imani na kwa hivyo tunahesabiwa wenye haki.

Wakati tunaokolewa kwa imani ndani ya Kristo, hatutahukumiwa; kifo chake kinatuondoa katika hukumu ya Mungu. Wakati tunakuja kwake kwa imani, tunahakikishiwa wokovu wetu kuwa ni wa milele.

Hii haimaanishi kwamba maisha ya ukristo ni rahisi na ni bila matatizo. Hata kama tunaondolewa katika hukumu ya Mungu, ulimwengu bado unatuchukia sana. Ulimwengu utajaribu kutushitaki. Hii ndiyo sababu Biblia inasema, “Ni nani atakayewashtaki wale ambao Mungu amewachagua? Ni Mungu mwenye ndiye mwenye kuwahesabia haki” (Warumi 8:33). Tena Biblia inasema, “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni shida au taabu au mateso au njaa,au uchi au hatari au upanga?” (Warumi 8:35). Jibu ni kwamba hakuna chochote kwa vitu hivi ambacho kinaweza kututenganisha na Mungu. Lakini katika mambo hayo yote, “Tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa Yeye aliyetupenda” (Warumi 8:37).

Mara mingi ulimwengu utatuchukia sana na mara mingi wakristo watakufa kwa ajili ya imani yao. Lakini hata wakifa wako na ahadi hii kutoka kwa Mungu: “Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani awezaye kuwa kinyme chetu?” (Warumi 8:31). Hata kama ulimwengu unatuchukia, tusife moyo. Sisi ni wenye haki machoni pa Mungu kupitia kwa imani ndani ya Kristo Yesu. Kristo alikufa kwa ajili yetu na Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu kwa ajili yetu. Sisi tuko hai ndani mwake na hakuna hukumu kwetu. “Wenye haki ni wajasiri kama simba” (Mithali 28:1).