Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili atulete kwa Mungu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Bring Us to God

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 22 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Kwa kuwa Kristo naye aliteswa mara moja tu, mwenye haki
kwa ajili ya wasio haki, ili awalete ninyi kwa Mungu”
(1 Petro 3:18).

“Lakini sasa, katika Kristo Yesu ninyi ambao hapo kwanza
mlikuwa mbali na Mungu, sasa mmeletwa karibu kwa njia ya
damu ya Kristo” (Waefeso 2:13).

Ujumbe wa ukristo ni injili ambayo ni habari njema. Katika Biblia habari njema ni Mungu mwenyewe na yale ambayo amefanya. Habari njema ni kwamba Mungu ametengeneza njia kwa watu wake waweze kuokolewa na wapatanishwe naye.

Kwa hivyo ujumbe wa ukristo unatuongoza kwa Mungu mwenyewe. Ikiwa tutahubiri ujumbe ambao hatuongozi kwa Mungu, basi hatuhubiri ukweli. Kwa hivyo wokovu ni habari njema kwa sababu tunaongozwa kwa Mungu na kutuletwa katika ushirika na Mungu wa milele. Ujumbe muhimu wa Biblia ni kwamba ndani ya Kristo Yesu, tuna ushirika wa milele na Mungu. Mungu ndiye msingi wa imani ya kikristo na ni yeye ndiye msingi wa wokovu wetu. Ikiwa hatutashiriki na Mungu, basi maisha hayana maana.

Huu ni ukweli ambao tunafaa kuzingatia sana. Kuna watu wengi ambao wanadai kuwa wameokoka na wanazungumza kuhusu msamaha wa dhambi, lakini hawazungumzi mengi kumhusu Mungu na ushirika naye. Wanajua kwamba wao ni watenda dhambi ambao wanamhitaji Mungu au si hivyo waelekee jahanum. Kwa hivyo wanakimbia kwa Kristo Yesu awakomboe kutoka kwa jahanum. Lakini hawaishi maisha matakatifu ambayo yanampendeza Mungu, kwa sababu kwao ushirika na Mungu siyo jambo la maana. Watu kama hawa wanahitaji kuuchunguza wokovu wao vizuri. Mtu ambaye hana haja na ushirika wa kila siku na Mungu na hajitahidi kuwa mtakatifu, mtu huyo hajaokoka. Sababu ya Kristo kufa ilikuwa atupatanishe na Mungu (1 Petro 3:18).

Sababu ya ujumbe huu kuwa habari njema ni, mwanadamu aliumbwa kuwa katika ushirika na Mungu. Hadi tutakapokuwa na ushirika na Mungu hatutawahi kutosheka na kila wakati tutakuwa tukitafuta furaha. Wakati tumekuja kwa Mungu na kuwa na ushirika naye, ndipo tutakuwa na furaha katika mioyo yetu.

Hili ni jambo ambalo watu wa Agano la Kale walijua vizuri. Daudi alijua njia hii na akasema, “Umenijulisha njia ya uzima; utanijaza furaha katika uwepo wako, pamoja na furaha za milele katika mkono wako wa kuume” (Zaburi 16:11). Mbele za uso wa Mungu kuna furaha tele. Hii ndiyo sababu Kristo alikufa, kutupatanisha na Mungu. Kristo alikuja kuleta furaha na kutosheka kwetu. Hii ndiyo sababu tunafaa kugeuka kutoka katika dhambi za kitambo (Waebrania 11:25) na tuje kwa furaha za milele. Njoo kwa Yesu.