Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili atuondoe katika hukumu wa mwisho

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Rescue Us from Final Judgment

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 47 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Vivyo hivyo Kristo alitolewa mara moja tu kuwa dhabihu ili
azichukue dhambi za watu wengi, naye atakuja mara ya pili, si ili
kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngoja
kwa shauku” (Waebrania 9:28)

Wakati Biblia inazungumza kuhusu wokovu, inazungumza kuhusu wokovu ambao tayari tumepewa, wokovu ambao tunapewa, na wokovu ambao tutapewa. Biblia inasema, “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani” (Waefeso 2:8). Pia inasema kwamba injili ndiyo “Lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu” (1 Wakorintho 1:18). Inaendelea kusema kwamba, “Sasa wokovu wetu umekaribia zaidi kuliko hapo kwanza tulipoamini” (Warumi 13:11). Kwa ufupi Biblia inafunza kwamba tumeokolewa, tunaokolewa na tutaokolewa.

Katika wokovu huu tunaokolewa na kifo cha Bwana Yesu Kristo. Tumeokolewa kwa sababu Bwana Yesu Kristo alitulipia fidia ya dhambi zetu na akatusamehe. Tunaokolewa kutoka kwa dhambi ambazo bado ziko mioyoni mwetu. Dhambi hizi zinaondolewa na Roho Mtakatifu ambaye Kristo alituma baada ya kupaa mbinguni. Siku ya hukumu tutaokolewa kwa sababu Kristo Yesu alikufa kwa ajili yetu na anatulinda kutokana na hukumu na hasira ya Mungu.

Kuna hukumu ambayo inakuja. Biblia inasema, “Lakini kinachobaki ni kungoja kwa hofu hukumu ya moto uwakao utakaowaangamiza adui za Mungu” (Waebrania 10:27). Biblia inatusihi “Tumwabudu Mungu kwa namna inavyompendeza, kwa unyenyekevu na uchaji, kwa kuwa ‘Mungu wetu ni moto ulao’” (Waebrania 12:28-29).

Yohana mbatizaji aliwaonya watu wa siku zake kuhusu hasira itakayokuja (Mathayo 3:7). Siku ya hukumu, “na kuwapa ninyi mnaoteseka raha pamoja na sisi, wakati Bwana Yesu atakapodhihirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. Atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na ambao hawakutii Injili ya Bwana wetu Yesu. Wataadhibiwa kwa uangamivu wa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa uweza Wake.” (2 Wathesalonike 1:7-9).

Biblia ni wazi kwamba adhabu ya watenda dhambi kule jahanum ni kali sana na ni ya kutisha. Yule ambaye hajaokoka, “Atakunywa mvinyo wa hasira kali ya Mungu ambayo imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yake pasipo kuchanganywa na maji. Naye atateswa kwa moto uwakao na kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele za Mwana-Kondoo” (Ufunuo 14:10-11).

Tunapojua jinsi adhabu ilivyo kali, basi tunajua ukuu wa wokovu wetu na, “Kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, yaani, Yesu, Yeye aliyetuokoa kutoka katika ghadhabu inayokuja” (1 Wathesalonike 1:10). Ni Bwana Yesu Kristo pekee ambaye anaweza kutuokoa kutokana na hasira ya Mungu ambayo inakuja. Bila Yeye tutaangamia.

Wale ambao wameokoka wanajua kwamba wakati Kristo atakaporudi watakuwa salama kwa sababu wameokolewa kwa damu yake. “Vivyo hivyo Kristo alitolewa mara moja tu kuwa dhabihu ili azichukue dhambi za watu wengi, naye atakuja mara ya pili, si ili kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngoja kwa shauku” (Waebrania 9:28). Kristo ameangamiza dhambi mara moja na alishinda. Hatuhitaji sadaka nyingine yoyote. Ngao yetu dhidi ya hasira ya Mungu na hukumu wa Mungu ni Kristo Yesu. Aliteseka na akafa kwa niaba yetu.