Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili atupatanishe na Mungu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Reconcile Us to God

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 21 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Kwa kuwa kama tulipokuwa adui wa Mungu tulipatanishwa
naye kwa njia ya kifo cha Mwanawe, si zaidi sana tukiisha
kupatanishwa tutaokolewa kwa uzima Wake” (Warumi 5:10)

Dhambi imeleta uadui kati ya mwanadamu na Mungu. Wakati Mungu na mwanadamu wanapatanishwa mambo mawili yanatendeka. Kwanza kabisa mawazo ya mwanadamu juu ya Mungu hubadilika kabisa. Mwanadamu ni mwasi dhidi ya Mungu na ni adui wa Mungu hadi wakati anapookolewa. Pili, Mawazo ya Mungu juu ya mwanadamu hubadilika kabisa. Mungu amekasirika kwa sababu ya dhambi za mwanadamu, na hasira hii lazima iondolewe. Njia moja tu ambayo mawazo ya Mungu yanaweza kubadilishwa ni, hadi Mungu mwenyewe ambadilishe mwandamu. Hadi Mungu mwenyewe afanye hivi, mwanadamu ataendelea kuwa adui wa Mungu. Sisi ni waasi wa Mungu na maadui wake, na tutaendelea kuwa maadui hadi Mungu mwenyewe afanye kazi katika mioyo yetu na atubadilishe. Hadi afanye kazi hiyo hatutawahi kubadilika; tutaendelea kuwa maadui wake.

Biblia inatuambia kwamba Mungu hufanya kazi hii ndani mwetu wakati bado tuko maadui. Kwa ufupi Biblia inasema kwamba Mungu hutupatanisha naye wakati sisi ni maadui wake. Biblia inasema hivi kuhusu wale ambao hawajaokoka, “Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui na Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii” (Warumi 8:7). Hii ndiyo ilikuwa hali ya kila mwanadamu wakati Mungu alimtuma Kristo katika ulimwengu huu atuokoe. Alikufa kwa ajili yetu ili aondoe hasira ya Mungu, na Mungu aweze kupatanishwa na watenda dhambi. Kwa kifo cha Kristo msalabani, aliwaondolea watu wake hatia na akafungua njia ya wateule kushiriki na Mungu. “Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi Yake mwenyewe, akiwa hawahesabii watu dhambi zao” (2 Wakorintho 5:19).

Hii ndiyo sababu wahubiri wa injili wanawaambia watenda dhambi, “Twawaomba sasa ninyi kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu” (2 Wakorintho 5:20). Kile wanamaanisha na haya ni kwamba, “Kuja kwa Yesu na ataondoa dhambi zako na uchafu wako na atakupatanisha na Mungu.”

Biblia inazungumza kuhusu upatanisho kati ya mwanadamu na mwanadamu. Biblia inasema hivi kuhusu hali hii, “Kwa hiyo, kama utaona sadaka yako madhabahuni, ukakumbuka kuwa ndugu yako ana kitu dhidi yako, iache sadaka yako hapo hapo, mbele ya madhabahu, uende kwanza ukapatane na ndugu yako wa kiume au kike, kisha urudi na ukatoe sadaka yako” (Mathayo 5:23-24). Wakati Yesu Kristo anasema kwamba, “Upatane kwanza na ndugu yako,” anamaanisha kwamba tatua ile shida ambayo ndugu yako ako nayo dhidi yako. Kwa njia hiyo hiyo wakati tunapatanishwa na Mungu, dhambi zetu lazima ziondolewe kabisa. Hadi dhambi zetu zitakaposamehewa, hatuwezi kupatanishwa na Mungu.

Biblia inatuambia kwamba wakati Bwana Yesu Kristo alikufa msalabani, aliziondoa dhambi zetu ambazo zilikuwa kinyume na Mungu. Kwa hivyo sasa Mungu hatarajii tulipe chochote kwa ajili ya dhambi zetu au kufanya matendo ambayo tunawaza kwamba yatuletea wokovu. Kristo Yesu amefanya kila kitu ambacho tunahitaji ili tupatanishwe na Mungu. Tunahitaji tu kuja kwa Kristo Yesu kwa imani.