Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili atusafishe dhamira zetu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Give Us a Clear Conscience

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 16 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Basi si zaidi sana damu ya Kristo, ambaye kwa Roho wa milele
alijitoa nafsi Yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na waa
kutusafisha dhamiri zetu, kutokana na matendo yaletayo mauti,
ili tupate kumtumikia Mungu aliye hai!” (Waebrania 9:14).

Wakati Adamu na Hawa walipoanguka katika dhambi, walifanyika wenye dhambi na wenye hatia. Dhambi yao iliharibu kila kitu na walijua jambo hili na kwa hivyo walishikwa na aibu. Dhambi yao iliharibu ushirika wao na Mungu, ndiyo sababu walijificha kutoka kwake. Dhambi hiyo iliharibu uhusiano wao wawili ndiyo sababu walianza kulaumiana. Pia dhambi yao iliharibu amani ambayo walikuwa nayo na wakawa na aibu.

Watu wa Mungu katika Agano la Kale walikuwa na shida hii wote. Walijua kwamba wametenda dhambi dhidi ya Mungu na dhamira yao iliwahukumu. Sadaka za wanyama ambazo walikuwa wakileta hekaluni hazikuondoa hatia ya dhamira zao. “Huu ulikuwa mfano kwa ajili ya wakati wa sasa, kuonyesha kwamba sadaka na dhabihu zilizokuwa zikitolewa hazikuweza kusafisha dhamiri ya mtu anayeabudu. Lakini hizi zilishughulika tu na vyakula na vinywaji pamoja na taratibu mbalmbali za kunawa za nje, kanuni kwa ajili mwili zilizowekwa hadi wakati utimie wa matengenezo mapya” (Waebrania 9:9-10). Wanyama ambao waliletwa kama sadaka katika hekalu waliosha tu nje ya mwili lakini siyo dhamira.

Hakuna damu ya mnyama ambayo ingeweza kuosha dhamira, na watu walielewa jambo hili (Isaya 53 na Zaburi 51). Hili ni jambo ambalo hata sisi tunajua: damu ya mnyama haiwezi kutupatia amani na Mungu. Hii ndiyo sababu Bwana Yesu Kristo alikuja kuwa kuhani mkuu zaidi. Alileta sadaka bora zaidi: siyo mnyama bali Yeye mwenyewe. “Basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo kuwa na mawaa, itawasafisha dhamira zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai (Waebrania 9:14). Kifo cha Bwana Yesu Kristo kinatuletea wokovu kwa kila mtu ambaye anamwamini. Hata watu wa Agano la Kale waliokolewa kupitia kwa kifo chake.

Hata leo shida ya mwanadamu ni ile ile: tunajua kwamba tumetenda dhambi dhidi ya Mungu na dhamira zetu hazina amani. Tunajihisi kwamba hatuna uzuri wowote kuja kwa Mungu.

Kuna watu wengi ambao hujaribu kufanya matendo mengi mazuri kwa tumaini kwamba matendo yao mazuri yatawawezesha kuja mbele za Mungu. Lakini hata baada ya kufanya matendo haya, bado wanajihisi kwamba dhambi zao haziwaruhusu kuwa katika ushirika na Mungu; dhamira zao haziwaletei amani. Yesu alisema kile ambacho kinatoka katika mwanadamu ndiyo kinacho mfanya awe mwenye dhambi (Marko 7:15-23). Ni kiburi chetu na tamaa zetu na hasira zetu na uchungu wetu, mambo haya ndiyo yanatufanya kuwa watenda dhambi. Haya yote ni mambo ambayo yanatoka katika moyo wenye dhambi na yanaitwa matendo mafu kwa sababu yanatoka katika moyo ambao umekufa kwa Mungu na hauna maisha ndani mwake.

Dawa kwa dhamira ambayo inasumbuka ni damu ya Kristo Yesu. Wakati tunakuja kwa Kristo Yesu, damu yake inatuosha kutokana na dhamira chafu na kutuleta katika amani na Mungu. Ndiyo njia ya pekee tunaweza kuwa na amani na ushirika na Mungu.