Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili atuwezeshe kuishi kwa ajili Yake bali siyo kwa ajili yetu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Enable Us to Live for Christ and Not Ourselves

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 32 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Naye alikufa kwa ajili ya watu wote, ili kwamba wote
wanaoishi wasiishi tena kwa ajili ya nafsi Yake Yeye aliyekufa na
kufufuka tena kwa ajili yao.” (2 Wakorintho 5:15).

Msitari huu unaopatikana katika kitabu cha 2 Wakorintho 5:15 unasema kwamba Kristo alikufa ndipo wale ambao wameokoka wamwishie. Yaani, alikufa ili tumtukuze yeye na kumwinua.

Biblia inatueleza wazi kwamba wakati tunaishi maisha ya dhambi huwa tunakosa kumletea Mungu utukufu (Warumi 3:23). Lakini Kristo alikufa ili aondoe dhambi zetu na atukomboe kutoka kwa dhambi ili tusiishi maisha ya dhambi bali tumwishie Kristo. Yesu alikufa ili tuachiliwe kutoka kwa dhambi na tuishi maisha ya kumtukuza.

Kuishi maisha ya kumtukuza Kristo ndilo jambo muhimu sana mtu anaweza kufanya hapa duniani. Bwana Yesu Kristo ni Mungu, na ni mkamilifu katika kila jambo, ni mwenye hekima, ni mwenye haki na huadhibu dhambi. Pia ni Mungu mwenyewe ambaye ako na nguvu zote. “Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi Yake” (Waebrania 1:3). Kwa hivyo jambo mzuri maishani ni kumpenda na kumtumikia Kristo na kuishi tukimtukuza.

Mtume Paulo aliandika: “Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, sasa nayahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara tupu nikiyalinganisha na faida kubwa ipitayo kiasi ya kumjua Kristo Yesu Bwana wangu, ambaye kwa ajili Yake nimepata hasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nimpate Kristo” (Wafilipi 3:7-8).

Wakati tunasema ni lazima tumtumikie Kristo, haimaanishi kwamba Kristo hawezi kufanya chochote bila sisi. “Wala hatumikiwi na mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji cho chote” (Matendo ya Mitume 17:25). Si kweli kwamba bila sisi Kristo hawezi kufanya lolote. “Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai Wake kwa ukombozi kwa ajili ya wengi” (Marko 10:45). Yesu Kristo alikufa ili tuweze kuona utukufu wake. Alikufa ili atutoe kutoka kwa utumwa wa dhambi ili tuwe na furaha ya kumtumikia.

Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba anaenda mbinguni ili amtume Roho Mtakatifu ambaye ni Msaidizi (Yohana 16:14). Aliwaambia wakati Roho Mtakatifu atakapokuja atamtukuza Yesu Kristo (Yohana 16:14). Kristo alikufa na akafufuka na pia akamtuma Roho Mtakatifu ili tuweze kuona utukufu wake. Hii ndiyo kazi Roho Mtakatifu hufanya, hutuonyesha utukufu wa Yesu Kristo. Hii ndiyo sababu Yesu aliomba, “Baba, shauku Yangu ni kwamba, wale ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili waweze kuuona utukufu Wangu, yaani, utukufu ule ulionipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu” (Yohana 17:24). Ni kwa sababu hii Kristo alikufa.