Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili awapatie uzima wa milele wote ambao wanamwamini

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Give Eternal Life to All Who Believe on Him

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 19 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata
akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee,
bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).

Hakuna mwanadamu ambaye anataka kufa. Hata wakati mambo na hali ya maisha ni ngumu sana, huwa tunatazamia wakati ambao mambo yatakuwa mazuri. Kifo ni kitu ambacho huwa hatupendi.

Hii ni kwa sababu kifo ni kitu kibaya sana. Ni adui ambaye anatuondoa katika mambo ya ulimwengu huu, ndiyo mwisho wa tumaini letu la kuishi katika ulimwengu huu. Kila mmoja wetu anataka kuishi na hakuna mmoja ambaye ako tayari kufa.

Hivi ndivyo Mungu ametuumba. “Ameiweka hiyo milele katika ya mioyo ya wanadamu” (Mhubiri 3:11). Tumeumbwa katika mfano wa Mungu na Mungu anapenda maisha na anachukia kifo. Tuliumbwa kuishi milele na tutaishi milele. Kinyume cha maisha ya milele ni jahanum. Mara mingi Yesu alihubiri kuhusu jahanum. “Ye yote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake” (Yohana 3:36).

Bwana Yesu Kristo alifunza wazi kwamba jahanum ni ya milele: “Ndipo hawa watakapoingia kwenye adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele” (Mathayo 25:46). Hii ndiyo itatendeka kwa wale wote ambao wanakataa neno la Mungu. Watakuwa katika uchungu wa jahanum milele. Hii ndiyo sababu Yesu alisema, “Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, ling’oe. Ni afadhali kuwa chongo ikaingia katika Ufalme wa Mungu kuliko kuwa na macho mawili na ukatupwa jahanum. Mahali ambako funza wake hawafi, wala moto hauzimiki” (Marko 9:47-48).

Jahanum siyo kama dunia. Hapa duniani kuna matatizo mengi lakini pia kuna vitu vingi vizuri. Mbinguni kuna kila kitu kizuri na jahanum iko na kila kitu kibaya; hakuna anasa au furaha huko.

Wale ambao wameokoka watabadilishwa ili miili yao mipya iweze kufurahia mambo mazuri ya mbinguni: “Lile mambo ambalo jicho halijapata kuona, sikio halijapata kusikia, wala halikuingia moyoni lile Mungu alilowaandalia wale wampendao” (1 Wakorintho 2:9). Hili ni jambo la ukweli kwa wale wote ambao wanamwamini Kristo Yesu. Mbinguni tutaona utukufu wa Mungu. Na uzima wa milele ndio huu, “Wakujue wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yohana 17:3). Hii ndiyo sababu Kristo aliteseka na akakufa, na ni wale tu ambao watamwamini ndiyo watauona utukufu wa Mungu.