Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili awe kuhani mwenye huruma na mwenye usaidizi

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Become a Sympathetic and Helpful Priest

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 27 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Yeye mwenyewe alijaribiwa kwa kila namna, kama vile sisi
tujaribiwavyo, lakini Yeye hakutenda dhambi. Basi na tukikaribie
kiti cha rehema kwa uajasiri, ili tupewe rehema na kupata neema
ya kusaidia wakati wa mahitajii” (Waebrania 4:15-16).

Wakati Bwana Yesu Kristo alijitoa msalabani kwa ajili yetu, alifanyika kuhani wetu mkuu (Waebrania 9:26). Yeye ndiye anayetuakilisha kwa Mungu. Kifo chake msalabani kilimfurahisha Mungu, kwa hivyo Mungu hatawahi kumkataa wakati anatuakilisha. Kwa hivyo tunapoenda kwa Mungu kupitia kwake Mungu hatatukataa.

Lakini Bwana Yesu Kristo ni zaidi ya sadaka yetu. Aliishi hapa ulimwenguni kwa miaka zaidi ya 30. Wakati huo wote alikumbana na majaribu na mateso kama jinsi sisi tunavyokumbana nayo. Yesu Kristo hakuwahi tenda dhambi lakini alipatana na majaribu ambayo tunapatana nayo. Majaribu ambayo alikutana nayo yalikuwa magumu sana kuliko yale ambayo tunakutana nayo leo kwa sababu shetani alijaribu sana kumfanya Kristo atende dhambi. Yesu Kristo alivumilia hadi mwisho na hakuna wakati alishindwa. Kwa hivyo anajua inamaanisha nini kujaribiwa.

Hii inamaanisha kwamba Bwana Yesu Kristo ana uwezo wa kutuhurumia wakati tunajaribiwa. Aliishi maisha ya kujaribiwa. Alijaribiwa kwa kila hali lakini hakuna wakati alishindwa. Biblia inasema, “Yeye hakutenda dhambi, wala udanganyifu haukuonekana kinywani mwake. Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano, alipoteswa, hakutishia, bali alijikabidhi kwa Yeye ahukumuye kwa haki” (1 Petro 2:22-23).

Kwa hivyo Biblia inasema kwamba anaweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu (Waebrania 4:15). Mwana wa Mungu ambaye amekalia mkono wa kuume wa Mungu anaelewa inamaanisha nini kuhisi uchungu, kushushwa moyo na kujaribiwa kutenda dhambi.

Ukweli huu uko na muhimu mkubwa sana ikizingatiwa zaidi hali yetu. Ukweli huu unamaanisha kwamba tunaweza kuja kwa Kristo kwa maombi kwa sababu Biblia inasema kwamba, “Yeye mwenyewe alijaribiwa kwa kila namna, kama vile sisi tujaribiwavyo, lakini Yeye hakutenda dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha rehema kwa uajasiri, ili tupewe rehema na kupata neema ya kusaidia wakati wa mahitaji.” (Waebrania 4:15-16).

Mara mingi kuna watu ambao huwaza kwamba wakija kwa Mungu na udhaifu wao, basi Mungu hatawakubali. Wanajua kwamba Mungu ni mtakatifu na wao wenyewe ni wenye dhambi na mbele yake hawana amani. Lakini wanapokumbuka kwamba Bwana Yesu Kristo anajua udhaifu na mateso yao, watapata ujasiri wa kukumbana na majaribu yao. Tunajua kwamba hatatukataa bali anaelewa yale ambayo tunapitia.