Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili awe kwetu mahali ambapo tunakutana na Mungu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Become for Us the Place Where We Meet God

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 25 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


‘Yesu akawajibu, “Libomoeni hili hekalu, nami nitalijenga tena
kwa siku tatu!”’ (Yohana 2:19-20)

Bwana Yesu Kristo alikufa ili awe mahali ambapo Mungu anakutana na watu wake. Hii ndiyo sababu Yesu alisema kwamba, “Nitaiharibu hekalu hii na kwa siku tatu nitaifufua.” Wakati alisema maneno haya hakuwa anazungumza kuhusu jengo la hekalu la Yerusalemu bali alikuwa anazungumza kuhusu mwili wake.

Yesu Kristo alikuja kuwa mahali ambapo Mungu na watu wake wangekutania. Wakati Bwana Yesu Kristo alikufa msalabani, hekalu na sadaka zilifika kikomo. Mambo haya yote yalipita.

Bwana Yesu Kristo ndiye mahali bora zaidi kuliko hekalu pa kukutana na Mungu. Yesu alisema, “Mkuu kuliko Hekalu yupo hapa” (Mathayo 12:6). Katika Agano la Kale Mungu mwenyewe angekuja katika hekalu lakini si kila wakati. Lakini kuhusu Kristo Yesu Biblia inasema kwamba, “Maana ukamilifu wote wa uungu umo ndani ya Kristo katika umbile la mwili wa kibinadamu” (Wakolosai 2:9). Bwana Yesu Kristo mwenyewe ni Mungu, tunapokutana naye, tunakutana na Mungu.

Katika Agano la Kale kulikuwa na makuhani ambao walikuwa wanadamu wa kawaida, yaani, wenye dhambi kama kila mtu. Biblia inasema hivi kumhusu Bwana Yesu Kristo: “Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani, mwanadamu Kristo Yesu” (1 Timotheo 2:5). Ikiwa unataka kutana na Mungu, kuna njia moja tu: kupitia kwa Kristo Yesu. Hatuhitaji jengo la kanisa au mchungaji au kasisi au mtu yeyote, tunahitaji Kristo Yesu pekee.

Katika Biblia tunasoma wakati mmoja ambao Kristo Yesu alizungumza na mwanamke msamaria. Mwanamke msamaria alimwambia Kristo, “Baba zetu waliambudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu. Yesu akamjibu, “Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu. Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi. Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta” (Yohana 4:20- 23).

Hapa Kristo Yesu anafunza kuhusu kuabudu kwa ukweli. Kuabudu kwa kweli hakuhusu ni wapi unaabudia, kwa mlima au kanisani, bali kwa roho na kweli. Katika mji wa Yerusalemu hakuna lile jengo la hekalu leo. Yerusalemu siyo mahali ambapo tunakutana na Mungu. Ikiwa tunataka kumwona Mungu, lazima tuende kwa Kristo Yesu kwa sababu yeye mwenyewe alisema, “Aliyeniona mimi, amemwona Baba” (Yohana 14:9). Ikiwa tunataka kumpokea Mungu lazima tumpokea Kristo kwa sababu alisema, “Anipokeaye mimi, amempokea Yeye aliyenituma” (Mathayo 10:40). Ikiwa tunataka Mungu awe miongoni mwetu wakati tunamwabudu, basi lazima tumtafuta Kristo. Kristo alisema, “Anayemkubali Mwana anaye Baba pia” (1 Yohana 2:23). Ikiwa tunataka kumheshima Baba lazima tumheshimu Kristo. Kristo alisema kwamba, “Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyemtuma” (Yohana 5:23). Wakati Kristo alipokufa na kufufuka alichukua nafasi ya hekalu. Unaweza kuja kwake wakati wowote na mahali popote, siyo tu kanisani.