Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili msalaba wake uwe majivuno yetu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Make His Cross the Ground of All Our Boasting

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 33 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Mungu apishie mbali nisije nikajivunia kitu cho chote
isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa
Yeye ulimwengu umesulubiwa kwangu, nami nimesulubiwa kwa
ulimwengu” (Wagalatia 6:14).

Biblia inatuambia kwamba wale wameokoka wanafurahia msalaba kwa sababu ndiyo njia ya wokovu. Inasema tunapaswa “kufurahi katika utukufu wa Mungu” (Warumi 5:2), “katika dhiki pia” (Warumi 5:3), “katika udhaifu” (2 Wakorintho 12:9) na “katika Kristo” (1 Wathesalonike 2:19). Lakini zaidi ya yote tunanapaswa kufurahia katika msalaba wa Yesu.

Sababu ya sisi kufurahia ndani ya msalaba wa Yesu Kristo ni kuwa, huu ndiyo msingi wa imani yetu. Kila kitu kingine hutoka hapa. Tunafurahia wakati wa shida na wakati wa udhaifu wetu kwa sababu ya msalaba. Haingekuwa msalaba wa Yesu hatungefurahia mambo haya.

Biblia inatufundisha kwamba msalaba wa Yesu Kristo hubadilisha kila kitu. Ikiwa mtu hajaokoka atapata hawezi kufurahia msalaba, hawezi akasema kwamba jambo fulani muhimu limemtendekea na kwamba amepata baraka kutoka kwa Mungu. Jambo moja tu atasema ni kwamba yeye ako na shida mingi maishani.

Lakini mtu ambaye ameokoka hufurahia baraka nyingi kutoka kwa Mungu kwa sababu ya kifo cha Yesu Kristo. Hata zile shida anazopata katika dunia hii ni baraka kwake.

Hii inamaanisha kwamba wakristo wanapaswa kukua jinsi wanavyokumbana na mambo. Ikiwa mkristo atakumbwa na matatizo ya maisha, hapaswi kulalamika kama mtu wa dunia bali anapaswa kuwaza kulingana na Biblia kuhusu shida alizo nazo. Anapaswa kuufikiria msalaba wa Kristo na pia anapaswa akumbuke yeye si mtu wa dunia: “Ulimwengu umesulibishwa kwangu, na nimesulubiwa kwa ulimwengu” (Wagalatia 6:14). Hadi wakati tutafikiria na kutembea katika ukweli wa yale ambayo yalitendeka msalabani, ndipo tunaweza kuishi maisha ya ukristo.

Kwa hivyo wakati mtu ameokoka ulimwengu huwa haumpendezi kamwe. Yeye amekufa kwa mambo ya ulimwengu huu na hayafuati, yeye ni “Kiumbe kipya” (Wagalatia 6:15). Yeye amezaliwa upya katika imani ndani ya Yesu Kristo. Wakati mtu amekuwa kiumbe kipya, anaishi maisha ya kumtumikia Kristo na anaanza kuziacha kabisa anasa za dunia hii. Anajua kwamba anaenda mbinguni kuwa na Yesu Kristo na kwa hivyo anaanza kutilia maanani sana mambo ya Kristo na ufalme wa Mungu.