Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili tuhesabiwe haki

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Provide the Basis for Our Justification

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 10 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Basi, kwa kuwa sasa tumehesabiwa haki katika damu yake”
(Warumi 5:9).

“Wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya
ukombozi ulio katika Kristo Yesu” (Warumi 3:24).

“Mwanadamu huhesabiwa haki kwa njia ya imani wala si kwa
matendo ya sheria” (Warumi 3:28).

Mtu ambaye ako huru ni mtu ambaye amesamehewa dhambi zake zote. Kwa mfano, mtu akipelekwa kotini ili ahukumiwe. Kotini hakimu husikiza mashtaka ya mtu huyu na ushuhuda. Halafu baada ya kusikiza, anasema ushuhuda siyo dhabiti, huyu mtu hana makosa na yuko huru kwenda.

Kufanywa huru ni kitu ambacho hutendeka katika mahakama ya sheria. Hakimu anaposema hana makosa anamaanisha mtu huyo hawezi kuendelea kuzuiliwa gerezani.

Bibilia inatufundisha ya kuwa wakati Mungu anatuokoa, yeye huwa anatusamehea dhambi zetu zote. Hii inamaanisha ya kuwa yeye huhakikisha kwamba sisi ni wasafi mbele yake.

Katika mahakama ya sheria, ikiwa mtu anaachiliwa huru inamaanisha kwamba hana hatia yoyote ijapokuwa aliwekelewa mashtaka. Hakimu atapata ya kuwa hana hatia yoyote. Hii inamaana ya kuwa mtu huyu hakukeuka sheria kwa njia yoyote ile.

Lakini mbele ya macho za Bwana sisi wote ni wenye dhambi, tumekeuka sheria za Bwana. Kwa hivyo hatuwezi linganishwa na yule mtu aliye katika mahakama ya kisheria. Bibilia inasema ya kwamba, “Yeye asemaye asiye haki ana haki, naye asemaye mwneye haki hana haki, Bwana huwachukia sana wote wawili” (Mithali 17:15). Na Mungu huwaweka huru wanawo mwamini (Warumi 4:5). Kwa maneno mengine Mungu hufanya maajabu.

Bibilia inatuambia kwamba Mungu huchukua mtu mwenye dhambi kotini mwake na kumtangaza mwenye haki. Hii ni kwa sababu mtu huyu amemwamini Yesu Kristo na ameokolewa. “Na kwa hivyo Mungu anaweza kuwa mfanya haki kwa yule ambaye anayeamini Yesu” (Warumi 3:26). Kuna sababu mbili kwa nini Mungu anaweza kufanya hivi. Kwanza ni kwa sababu Yesu alikufa kulipa deni kwa ajili ya kila mtu atakayemwamini. “Tumehesabiwa haki kwa damu yake” (Warumi 5:9). Mtu huja kotini kama ana makosa. Ameishi maisha ya dhambi. Yesu atachukua rekodi hii ya dhambi na kulipa deni yake. Hii ndiyo sababu Mungu humtangaza mtu huru.

Sababu ya pili tutaangalia katika ukurasa unaofuatia.