Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili tusamehewe dhambi zetu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/For the Forgiveness of Our Sins

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 9 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Katika Yeye tunao ukombozi kwa njia ya damu Yake, yaani,
msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neeme Yake”
(Waefeso 1:7).

“Hii ndiyo damu yangu ya agano, ile imwagikayo kwa ajili ya
wengi kwa ondoleo la dhambi” (Mathayo 26:28).

Kwa kawaida mtu akitukosea, mara mingi sisi huwasamehe na huwa hatulipizi kitendo kilichotendwa dhidi yetu. Kwa mfano, mtoto akiharibu simu ya babake halafu babake amsamehe, baba huwa hatarajii mtoto kulipa simu yake. Baba akimwambia mtoto, “nimekusamehe,” anamaanisha ya kwamba mtoto amekosea lakini amemsamehe.

Hivi ndivyo Mungu hutusamehe ikiwa tutamwamini mwanawe Yesu Kristo na tuweze kukombolewa: “Kila mtu amwaminiye hupokea msamaha wa dhambi katika jina lake” (Matendo ya Mitume 10:43). Tunapokombolewa kupitia kwa Yesu Kristo, Mungu anatusamehe dhambi zetu zote. Hivi ndivyo Bibilia inavyosema: “Mimi ndimi nizifutaye dhambi zako, kwa ajili yangu mwenyewe” (Isaya 43:25); “Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo Mungu ameziweka dhambi zetu mbali na sisi” (Zaburi 103:12).

Tunafaa tuelewe kwamba kabla Mungu asamehe mtu inapaswa kuwa na fidia ambaye amelipwa. Ni kama mtu ambaye ameua mwingine na baadaye kumwambia hakimu, “Pole, nimeua mtu, tafadhali nisamehe.” Hakimu hawezi kumwachalia aende. Amemwua mtu na lazima aadhibiwe hata kama anasema pole.

Hivi ndivyo ilivyo na kila mtenda dhambi; ni lazima aadhibiwe kwa sababu ya dhambi zake. Dhambi zote ni mbaya kwa sababu ni uasi dhidi ya Mungu mwenyewe.

Hii ndiyo sababu Yesu aliteswa na akafa: “Kwa damu yake tunao ukombozi na msamaha wa dhambi” (Waefeso 1:7) Tunapoenda kwa Yesu kwa kumwomba msamaha, tunasamehewa kwa sababu Yesu amezilipia dhambi zetu. Msamaha ni zawadi ya bure kwetu kutoka kwa Mungu kwa sababu Yesu alitununulia zawadi hii.