Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili tuwe mali yake

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/So That We Might Belong to Him

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 23 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Vivyo hivyo, ndugu zangu, ninyi mmeifia sheria kwa njia ya
mwili wa Kristo, ili mweze kuwa mali ya wengine, Yeye ambaye
alifufuka kutoka kwa wafu, ili tupate kuzaa matunda kwa
Mungu” (Warumi 7:4)

“Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu
akaye ndani yenu, ambaye amepewa na Mungu? Ninyi si mali
yenu wenyewe, kwa maana mmenunuliwa kwa gharama. Kwa
hivyo, mtukuzeni Mungu katika miili yenu” (1 Wakorintho 6:19-20)

“Lichungeni kanisa lake Mungu alilolinunua kwa damu yake
mwenyewe” (Matendo ya Mitume 20:28)

Swali kuu tunafaa kujiuliza katika maisha yetu ni, mimi ni wa nani? Watu ulimwenguni hawaelewi kwamba wao ni watumwa. Wanawaza kwamba wao wako huru kufanya yale yote ambayo wanataka kufanya kwa sababu wao siyo wa mtu yeyote.

Bwana Yesu Kristo ako na maneno haya kwa watu wote wa ulimwengu huu: “Mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.” Wakati alisema maneno haya, wale ambao alikuwa akizungumzia maneno haya walisema, “Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru. Wao wakamjibu, ‘Sisi tu wazao wa Abrahamu, nasi hatujawa watumwa wa mtu ye yote. Wawezaje kusema kwamba tutawekwa huru?’ Yesu akajibu, ‘Amin, amin, nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.” (Yohana 8:32-34).

Biblia ni wazi kwamba hakuna mtu yeyote hapa ulimwenguni ambaye ako huru, sisi sote ni watumwa wa mtu fulani. Watu wengine ni watumwa wa dhambi, wengine ni watumwa wa Mungu. “Je, hamjui kwamba mnapojitoa kwa mtu ye yote kama watumwa watiifu, ninyi ni watumwa wa yule mnayemtii, aidha watumwa wa dhambi, ambayo matokeo yake ni mauti, au wa utii ambao matokeo yake ni haki...mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa hamtawali na haki...lakini sasa kwa kuwa mmewekwa huru mbali na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu” (Warumi 6:16, 20, 22).

Wakati Biblia inasema kwamba sisi ni watumwa wa dhambi inamaanisha kwamba hatuko huru kutii sheria ya Mungu na kuifuata. Hadi Mungu mwenyewe atupatie nguvu zake kupitia kwa Roho Mtakatifu ndipo tutaweza kumtii. Hii ndiyo sababu Biblia inasema kwamba, “Lakini Mungu ashukuriwe, kwa kuwa ninyi ambazo kwanza mlikuwa watumwa wa dhambi, mmeuwa watii kutoka moyoni kwa mafundisho mliopewa.” (Warumi 6:17). Wokovu ni kazi ya Mungu. “Mungu atawajalia kutubu na kuijua kweli, ili fahamu zao ziwarudie tena, nao waponyoke katika mtego wa Shetani ambaye amewateka wapate kufanya mapenzi yake” (2 Timotheo 2:25-26).

Ni kifo cha Kristo Yesu ambacho kilinunua watu wake kutoka kwa dhambi. “Ninyi si mali yenu wenyewe, kwa maana mmenunuliwa kwa gharama” (1 Wakorintho 6:19-20). Thamani ambayo alilipa ilikuwa damu yake: “Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Lichungeni kanisa lake Mungu alilolinunua kwa damu yake mwenyewe” (Matendo ya Mitume 20:28).

Wakati tunaokolewa, Kristo anatuweka huru. Hii haimaanishi kwamba sasa tunafaa kuishi maisha ya dhambi, bali inamaanisha kwamba sasa tuko huru kumtumikia Mungu. Tunakuwa na uhusiano na Bwana Yesu Kristo: “Vivyo hivyo, ndugu zangu, ninyi mmeifia sheria kwa njia ya mwili wa Kristo, ili mweze kuwa mali ya mwingine, Yeye ambaye alifufuka kutoka kwa wafu, ili kwamba tupate kuzaa matunda kwa Mungu” (Warumi 7:4).

Kristo aliteseka na akakufa ili tuweze kuwa huru kutoka kwa utumwa wa dhambi. Wakati tumeokolewa na kuwa wake, tunaanza kumtii kwa furaha. Wewe huko huru; yaani wewe ni wa Mungu au wa shetani.