Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili tuweze kufa kwa dhambi na tuishi kwa utakatifu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/That We Might Die to Sin and Live to Righteousness

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 30 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili juu ya
mti, ili kwamba, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tupate
kuishi kwa haki” (1 Petro 2:24).

Biblia inatuambia kwamba Yesu Kristo alikufa msalabani kwa sababu ya watu wake. Wale wameokoka hufa kwa dhambi. Kifo cha Yesu Kristo kilikuwa ni cha kulipia fidia watu wake kwa sababu ya dhambi zao. Hii inamaanisha kwamba hawatahukumiwa milele jahanum. Hii ndiyo sababu Yesu alisema “Nami ninawapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe” (Yohana 10:28). Biblia pia inasema “Ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).

Biblia pia inatufundisha kwamba wale ambao wameokoka watakufa kwa dhambi kwa sababu Kristo alikufa kwa ajili yao: “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi” (1 Petro 2:24). Kristo alikufa ili tuwe na maisha ya milele na pia Kristo alikufa ili nasi tufe kwa dhambi. Hii ndiyo sababu Biblia inasema, “Tumeungana naye katika ufufuo Wake” (Warumi 6:5); “Mmoja alikufa kwa ajili ya wote, kwa hiyo wote walikufa” (2 Wakorintho 5:14).

Wale wamemwamini Yesu Kristo wameungana naye na wamekufa naye. Wakristo wote, “Wamesulibiwa pamoja na Kristo” (Wagalatia 2:20).

Wakati Yesu Kristo alikufa msalabani Kalivari alikufa kwa sababu ya dhambi zetu. Dhambi zetu ziliwekelewa juu yake, na akachukua nafasi yetu na akafa msalabani. Wakati mtu ambaye ameokoka anabatizwa, huwa anaonyesha kwamba amekufa kwa dhambi zake na amefufuka kwa maisha mapya ndani ya Yesu Kristo: “Tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti” (Warumi 6:4). Ubatizo ni ishara ya kuonyesha ni nini imefanyika ndani ya mtu wakati anaokoka. Maji ni kama kaburi, na yule anayeingizwa ndani ya maji tayari amekufa kwa dhambi zake na ubatizo ni ishara ya hii. “Mkiwa mmezikwa pamoja naye katika ubatizo na kufufuliwa pamoja naye kwa kuuamini uweza wa Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu.” (Wakolosai 2:12).

Mtu ambaye ameokoka amekufa kwa dhambi zake kwa sababu Kristo alimfia; “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake, juu ya mti, ili kwamba, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tupate kuishi katika haki” (1 Petro 2:24). Hii inamaanisha hatuishi tena jinsi tulivyokuwa tukiishi hapo zamani. Maisha ya dhambi tuliyokuwa tunayaishi kabla hatujaokoka ni lazima yakufe. Tunaanza maisha mapya: yaani tunakufa na kufufuka tena tukiwa tumeokoka.

Tunapookoka basi huwa tunakufa kwa maisha ya kale ya dhambi. Mtu ambaye aliishi maisha ya dhambi na kupenda dhambi ni lazima afe na Kristo Yesu. Mtu huyu dhambi kwake inakuwa si kitu cha kupendeza hata kidogo tena. Anajua kwamba ni dhambi yake ilimfanya Kristo akufe msalabani na ni lazima ayaache maisha yake ya dhambi. Sasa mtu huyu amekufa kwa dhambi na kamwe dhambi haimtawali. Dhambi sasa imekuwa adui wake.

Badala ya kuishi maisha ya dhambi, mkristo huyu anaanza kuishi maisha ya kumpendeza Mungu: “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake, juu ya mti, ili kwamba, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tupate kuishi katika haki.” (1 Petro 2:24). Dhambi inakuwa si ya kutamaniwa na mioyo yetu, na Kristo anakuwa ndiye wa kutamaniwa na mioyo yetu. Hivi ndivyo Biblia inasema, kwa kila mkristo, “Jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu Kwake kama vyombo vya haki.” (Warumi 6:13).