Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kukomboa watu ambao wako na hamu ya kufanya kazi ya Mungu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Create a People Passionate for Good Works

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 36 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote,
na kujisafishia watu wawe miliki yake mwenyewe, wale walio na
juhudi katika matendo mema” (Tito 2:14).

Ujumbe wa Biblia ni kwamba tumesamehewa makosa yetu yote na kwamba kumekubalika mbele za Mungu siyo kwa sababu tumefanya kazi mzuri lakini ni kwa imani ndani ya Kristo. Mungu anatuokoa bila malipo ndiyo tuweze kufanya mambo mazuri. Biblia inasema, “Ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu, si kwa matendo yetu mema” (2 Timotheo 1:9). Kwa hivyo kazi mzuri hazituokoi, tunafanya kazi mzuri baada ya kuokoka. Kazi mzuri ni matunda ya wokovu na siyo mizizi ya wokovu. Yesu Kristo alikufa, “Kujisafishia watu kuwa mali Yake Mwenyewe, yaani, wale walio na bidii katika kutenda mema.” (Tito 2:14).

Biblia inaeleza wazi kwamba wokovu ni kwa imani, siyo kitu ambacho tunapata kwa sababu tumefanya kazi. Ni zawadi tunapewa bila malipo kutoka kwa Mungu. Hii ndiyo sababu Biblia inasema, “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala hii si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu” (Waefeso 2:8-9). Yesu aliteseka na kufa ili kazi mzuri iwe ndiyo matunda ya imani ya ukristo wetu baada ya kuokolewa kwa imani.

Hii ndiyo sababu Biblia inasema, “Tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tupate kutenda matendo mema” (Waefeso 2:10). Hii inamaanisha tumeokolewa kwa imani ili tutende matendo mema baada ya kuokoka. Hii haimaanishi kwamba matendo mazuri ndiyo yanatuokoa, lakini matendo mazuri yanakuja baada ya kuokoka. Bwana Yesu Kristo hatupatii tu uwezo wa kutenda matendo mazuri, bali anatupatia bidii ya kufanya matendo mazuri. Hii ndiyo sababu Biblia inasema kwamba watu wa Mungu wanapaswa kuwa na juhudi ya kutenda matendo mema. Kuwa na juhudi juu ya jambo inamaanisha kutia bidii sana katika jambo hilo. Yesu alikufa ili tuwe na juhudi sana ya kufanya matendo mema. Yesu Kristo hataki tuwe na mioyo nusu nusu kuhusu matendo mazuri. Wale wameokoka wanapaswa kutia juhudi ya kuwa watakatifu kwa mioyo yao yote.

Sababu kuu kwa nini Yesu Kristo anataka tufanye matendo mema ni ili tuweze kumletea utukufu Mungu. Yesu alisema, “Nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.” (Mathayo 5:16). Wakati tunatenda matendo mema huwa tunamletea utukufu Mungu. Ni kwa sababu hii Kristo alikufa msalabani.

Wakati watu wa Mungu wanatenda matendo mazuri humu duniani, dunia huwa inayaona. Watu wa dunia ni watu wachoyo, hawafanyii wenzao matendo mazuri bali wanajifikiria tu wenyewe. Wakati wakristo wanawashughulikia wengine na kuwafanyia matendo mazuri Mungu huwa anatukuzwa.

Wakati Biblia inaongea kuhusu matendo mema, inamaanisha kuwasaidia wale wako na shida na mahitaji. Kwa mfano Biblia inasema, “Watu wetu hawana budi kujifunza kujitoa kutenda mema, ili waweze kuwasaidia watu wenye mahitaji ya lazima ya kila siku, wasije wakaishi maisha yasiyokuwa na matunda.” (Tito 3:14). Hii ndiyo sababu Kristo alikufa, ajisafishie watu wake wenye juhudi ya kutenda matendo mazuri, hasa hasa kuwasaidia maskini na wale wote ambao wako na mahitaji.