Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kuondoa ghadhabu ya Mungu
Kutoka Gospel Translations Swahili
By John Piper
About The Death of Christ
Chapter 1 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?
Translation by Desiring God
“Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa
kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikiwa,
‘Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti’” (Wagalatia 3:13).
“Yeye ambaye Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa
njia ya imani katika damu Yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki
Yake, kwa sababu kwa ustahimili Wake aliziachilia zile dhambi
zilizotangulia kufanywa” (Warumi 3:25).
“Huu ndio upendo, si kwamba tulimpenda Mungu, bali Yeye
alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili Yeye awe dhabihu ya
kipatanisho kwa ajili ya dhambi zetu” (1 Yohana 4:10).
Neno la Mungu linasema kwamba Mungu huhukumu dhambi. Linatuambia Mungu ni mtakatifu na ni lazima aadhibu wale wafanyao dhambi. Hii ndiyo sababu Yesu Kristo alikufa msalabani Kalivari. Neno la Mungu pia linatuambia kwamba Mungu ni wa upendo. Hii inamaanisha kwamba Mungu hapendi kizazi chote cha wanadamu kuhukumiwa jahanum. Kwa sababu Mungu ni mtakatifu hataruhusu watenda dhambi kuingia mbinguni. Kwa sababu ya upendo wake, Mungu alimtuma Yesu Kristo afe msalabani Kalivari kwa ajili ya dhambi za watu wake.
Sheria ya Mungu ni wazi. Inasema, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa nguvu zako zote” (Kumbukumbu la Torati 6:5). Lazima sisi wanadamu tutii sheria hii ya Mungu. Lakini ukweli ni kwamba hatumpendi Mungu, bali yake tunapenda vitu vingine kama pesa na anasa za dunia hii. Kwa kufanya hivi tunatenda dhambi dhidi ya Mungu. Hili ni jambo kila mwanadamu amelifanya. Hii ndiyo sababu neno la Mungu linasema, “Kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Hapa Biblia inazungumza juu ya kila mtu wala si watu fulani pekee.
Kwa hivyo dhambi siyo jambo dogo. Dhambi ni jambo kubwa kwa sababu ni uasi dhidi ya Mungu mwenyewe. Tunapofanya dhambi huwa hatumkosei mwanadamu bali Mungu mwenyewe. Wakati tunakosa kumtii Mungu, huwa tunamkosea heshima na tunajiletea hali ya kukosa furaha.
Biblia inatuambia kwamba Mungu huadhibu dhambi. Hii inamaanisha Mungu hatapuuza dhambi ya mtu yeyote. Mungu hukasirika kwa sababu ya kila dhambi tunayofanya na anaamuru fidia ilipwe kwa kila dhambi tunayofanya. “Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa” (Ezekieli 18:4). Biblia inatuambia wazi kwamba kuna laana juu ya kila mtu mtenda dhambi. Mungu ni mtakatifu na ni msafi. Hawezi akafunga macho yake wakati anaona dhambi ikifanywa. Ni lazima alaani kila dhambi. Biblia inasema kwamba, “Amelaani mtu yule asiyeshika na kutii mambo yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria” (Wagalatia 3:10; Kumbukumbu la Torati 27:26).
Biblia inatuambia kwamba Mungu ni Mungu ni Mtakatifu na pia ni Mungu wa upendo. Mungu hangekuwa wa upendo, watu wote wangetumwa jahanum. Lakini ukweli ni kwamba Mungu ni Mungu wa upendo na kwa hivyo alimtuma Yesu Kristo aje kutuokoa. Bwana Yesu Kristo alikuja ulimwenguni na akachukua laana ya watu wake: “Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kufanyika laana kwa ajili yetu” (Wagalatia 3:13).
Katika mwanzo wa sura hii tumenukuu mstari kutoka kwa kitabu cha Warumi 3:25 ambapo neno “upatanisho” lilitumika. Neno hili linamaanisha kutoa ghadhabu ya Mungu kwa kubandilishana na kitu kingine. Mungu alimtuma Yesu Kristo aje kufa kwa sababu ya watu wake. Wakati alikufa aliitoa ghadhabu ya Mungu ambayo ingeleta hukumu juu ya watu wake.
Ni muhimu sana kwetu wakati tunafikiria kuhusu upendo wa Mungu kuelewa kwamba hayo ni mambo yenye uzito sana. Upendo wa Mungu siyo tu hisia fulani nzuri Mungu ako nazo kwa watu wake. Upendo wa Mungu unadhihirika wakati Mungu mwenyewe alipomtuma Mwanawe aje kufa kwa sababu yetu na kuondoa ghadhabu ya dhambi zetu kutoka kwetu: “Huu ndio upendo, si kwamba tulimpenda Mungu, bali Yeye awe dhabihu ya kipatanisho kwa ajili ya dhami zetu” (1 Yohana 4:10).