Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kuonyesha upendo na neema ya Mungu kwa watenda dhambi

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Show the Wealth of God’s Love and Grace for Sinners

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 5 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mwenye haki; lakini
yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema.
Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa
kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye
dhambi” (Warumi 5:7-8).

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata
akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee,
bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).

“Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu,
masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake”
(Waefeso 1:7).

Kuna mambo mawili hapa ambayo yanaonyesha kwamba Mungu ako na upendo mkuu kwa wenye dhambi. Kwanza, tunaona upendo mkuu wa Mungu kwa wenye dhambi kwa sababu alimtuma Mwana wake aje kufa kwa ajili yetu: “Alimtoa Mwanawe wa pekee” (Yohana 3:16). Pili, tunaona upendo mkuu wa Mungu kwa wenye dhambi kwa vile sisi tuko wenye dhambi wakuu. Hatukuwa watu wazuri ndipo Yesu aje kukufa kwa sababu yetu, bali tulikuwa wenye dhambi wakuu machoni pa Mungu. Mambo haya mawili yanatuonyesha vile Mungu ako na upendo mkuu kwa sisi wenye dhambi.

Jina “Kristo” linamaanisha mtu muhimu sana, na mtu wa cheo kikuu. Agano la Kale linasema kwamba Kristo ni mfalme wa Waisraeli ambaye analeta amani kwa watu wa Mungu. Pia Agano la Kale linatueleza kwamba Kristo ni mfalme wa ulimwengu (Isaya 9:6-7).

Mtu yule Mungu alimtuma aje kufa kwa sababu yetu alikuwa mfalme mkuu. Alikuwa Mwana wake mwenyewe. Hii inaonyesha upendo mkuu wa Mungu kwa watu wake.

Watu wale Kristo alikufia walikuwa wenye dhambi. “Yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema - bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu” (Warumi 5:7-8). Tulikuwa wenye dhambi wakuu ambao walistahili kuhukumiwa wala si kuokolewa.

Mungu alimtuma Mwanawe ili afe kwa sababu ya “Wingi wa neema yake” (Waefeso 1:7). Yaani Mungu alimtuma Yesu Kristo kuja duniani ili tupate wokovu bila malipo. Hivi ndivyo upendo wa Mungu ulivyo mkuu, kwamba alimtuma Mwana wake afe kwa ajili yetu na anatupatia wokovu bila malipo.