Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kuonyesha upendo wake kwetu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Show His Own Love for Us

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 6 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda
ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa
Mungu, kuwa harufu na manukato” (Waefeso 5:2).

“Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake”
(Waefeso 5:25).

“Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana
wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu”
(Wagalatia 2:20).

Katika kifo cha Bwana Yesu Kristo, Mungu Baba alikuwa anaonyesha upendo mkuu kwa wateule wake (Yohana 3:16). Paulo alijua upendo huu wa Mungu kwake kupitia kwa Kristo Yesu: “Mwana wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu” (Wagalatia 2:20).

Wakati tunapofikiria kuhusu msalaba wa Kristo Kalivari, hivi ndivyo tunapaswa kufikiria: kila mtu ambaye ameokoka anapaswa kujua kwamba Kristo alikufa kwa ajili yake. Anapaswa kujua kwamba Kristo anampenda na alikufa kwa sababu yake. Anapaswa kukumbuka kwamba ni dhambi zake mwenyewe zilimtenganisha na Mungu. Anapaswa kukumbuka kwamba hajaokolewa kwa sababu ya mambo mazuri aliyoyafanya lakini ni kwa sababu Yesu Kristo alimhurumia.

Wakati tunawaza juu ya mateso na kifo cha Yesu, tunapaswa kujiuliza swali hili, “Kristo alikufa kwa ajili ya nani?” Jibu kutoka kwa Biblia ni, “Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake” (Waefeso 5:25). Pia Biblia inaendelea kusema, “Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake” (Yohana 15:13). Na, “Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi” (Mathayo 20:28).

Biblia inaeleza wazi kwamba Yesu Kristo alikufa kwa sababu ya watu wengi. Swali ambalo kila mtu anapaswa kujiuliza ni, “Je, mimi ni mmojawapo wa wale watakaofaidika na kifo cha Yesu?” Biblia inajibu swali hili hivi, “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka” (Matendo ya Mitume 16:31); “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokoka” (Warumi 10:13); “Kila mtu amwaminiye hupokea msamaha wa dhambi katika jina lake” (Matendo ya Mitume 10:43); “Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu” (Yohana 1:12); “Kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).

Wakati mtu anasoma maneno haya, Roho Mtakatifu humleta kwa Kristo. Anaona ndani ya Yesu mwokozi aliyekamilika na mtakatifu. Mtu anaona upendo wa Kristo juu yake na anasema,”Kristo alinipenda na akajitoa kwa ajili yangu” (Wagalatia 2:20).

Hii inamaanisha kwamba Kristo alilipa bei kubwa sana na alitununulia zawadi ya bei ghali sana. Hii ndiyo sababu alipokaribia kifo chake aliomba, “Baba, shauku Yangu ni kwamba, wale ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo” (Yohana 17:24). Wakati Yesu alikufa msalabani alituonyesha utukufu wa Mungu: “Nasi tukauona utukufu Wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli” (Yohana 1:14). Tunapoona upendo huu wa Yesu Kristo tunapaswa kuja kwake tukiwa tayari kuwa wafanya kazi wake na kuendelea kuona utukufu wa Mungu kupitia kwake.