Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kupatia ndoa maana yake halali

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Give Marriage Its Deepest Meaning

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 35 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo
alivyopenda Kanisa akajito akwa ajili yake..” (Waefeso 5:25).

Mungu amepanga ndoa kwamba mume atampenda mkewe kama vile Yesu Kristo anawapenda watu wake. Mke anapaswa kumtii mume kama vile watu wa Yesu wanapaswa kumtii yeye. Yesu alikuwa na sababu hii wakati alikuja kuwaokoa watu wake: alikuja kwa bibi arusi, kumpenda na kufa kwa sababu yake.

Hii haimaniishi kwamba mume anapaswa kufa ili amwokoe bibi yake, bali inamaanisha wanaume wapende wake zao jinsi Kristo alilipenda kanisa kwa njia maalum.

Mambo ya ndoa ni mambo ambayo Mungu alipanga kabla hajaumba Adamu na Hawa. Biblia inatufundisha kwamba wakati Mungu alianzisha ndoa, alikuwa anapanga kuhusu Kristo na kanisa wala si Adamu na Hawa. Hii ndiyo sababu Paulo anasema, “Kwa sababu hii, mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe na hawa wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hii ni kubwa, bali mimi nanena kuhusu Kristo na Kanisa.” (Waefeso 5:31-32).

Hii inamaanisha kutoka mwanzo Mungu alipanga ndoa ili aonyeshe uhusiano wa Kristo na kanisa lake. Uhusiano huu huonekana wazi wakati Kristo alikuja na kufa kwa sababu ya kanisa. Kwa hivyo tunapotazama ndoa kati ya mwanamume na mwanamke, tunaona uhusiano wa Kristo Yesu na kanisa lake.

Wakati Kristo alikufa msalabani Kalivari, alikuwa anawaza kuhusu watu wake. Yesu alijua wakati alikuwa anaenda msalabani kufa kwamba kifo chake kitawaonyesha watu wake maana ya kweli ya ndoa. Wakati aliteseka, alikuwa anawafundisha wanaume jinsi ya kuwapenda wake zao.

Tukiangalia duniani leo tunaona kwamba ndoa nyingi hazina raha. Hivi sivyo Mungu alikusudia, hili ni jambo ambalo lililetwa na dhambi. Dhambi imo mioyoni mwetu na hii ndiyo sababu wanaume hawapendi wake zao jinsi wanafaa kuwapenda. Pia kwa sababu hii wake hawawatii jinsi wanapaswa kutii waume zao. Yesu aliteseka na kufa ili aondoe dhambi hii. Na kwa sababu ya kifo chake Kristo Yesu, hatufai sasa kusema kwamba hata nisipompenda mke wangu au kumtii mume wangu jinsi ninafaa kumpenda ni kwa sababu ya dhambi. Kristo alikufa ili atuonyesha jinsi ya kuisha na wake na waume wetu. (Waefeso 5:22-25).