Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kuwa fidia ya watu kutoka kila kabila, rangi na taifa

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Ransom People from Every Tribe and Language and People and Nation

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 45 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Wewe unastahili kukitwaa kitabu na kuzivunja lakiri zake, kwa
sababu ulichinjwa na kwa damu Yako ukamnunulia Mungu watu
kutoka katika kila kabila, kila lugha, kila jamaa na taifa “
(Ufunuo 5:9)

Katika mstari huu tunatazama kile ambacho kinatendeka mbinguni. Mtume Yohana alikubaliwa kuona kile ambacho kitakuwa kikitendeka huku mbinguni milele. “Kisha nikaona katika mkono Wake wa kuume yule aliyeketi kwenye kiti cha enzi, kitabu kilichoandikwa ndani na upande wa nyuma kikiwa kimefungwa kwa lakiri saba.” (Ufunuo 5:1). Muhuri ni hesabu ya kila kitu ambacho kitatendeka hapa ulimwenguni. Moja wa malaika alimwambia Yohana, “Simba wa kabila la Yuda, wa uzao wa Daudi, ameshinda, ili kwamba aweze kukifungua hicho kitabu na kuvunja hizo lakiri zake saba” (Ufunuo 5:5). Simba wa kabila la Yuda ni Kristo Yesu. Ameshinda kifo, kwa kifo chake na kufufuka kwake. Yohana alimwona, “Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa” (Ufunuo 5:6).

Malaika wote waliaanguka chini na kuanza kumwabudu. Waliimba wimbo mpya wakisema kwamba kwa sababu Kristo Yesu alikufa, ako na uwezo wa kufungua muhuri wa kihistoria. Kile malaika hawa wanamaanisha ni kwamba, kwa sababu ya kifo cha Bwana Yesu Kristo, sasa Yeye ndiye Bwana wa kihistoria: Yeye anadhibiti kila kitu ambacho kinatendeka hapa ulimwenguni. Nao waimba wimbo mpya wakisema, “Wewe unastahili kukitwaa kitabu na kuzivunja lakiri zake, kwa sababu ulichinjwa na kwa damu Yako ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila, kila lugha, kila jamaa na taifa” (Ufunuo 5:9).

Kristo alikufa kuwaokoa watu wa aina tofauti kutoka kila taifa la ulimwenguni. Watu wa ulimwengu wametenda dhambi. Kila taifa ulimwenguni linahitaji wokovu. Hii ndiyo sababu Yesu Kristo alikuja ulimwenguni: alikuja kuwaokoa watu kutoka kila taifa la ulimwengu. Ugonjwa wa dhambi uko kila mahali na tabibu pia wa ugonjwa huu ako kila mahali. Kristo Yesu alisema, “Lakini Mimi, nikiinuliwa kutoka katika nchi, nitawavuta watu wote waje Kwangu.” (Yohana 12:32). Msalabani Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya watu kutoka kila taifa la ulimwengu.

Ukristo ulianza katika nchi ya Uisraeli na baadaye ukaenea bara Uropa. Sasa imeenea katika kila pembe la ulimwengu. Katika Agano la kale tunaambiwa kwamba hili jambo lilikuwa litendeke: “Miisho yote ya dunia watasherehekea na kuabudu, wote waendao mavumbini watapiga magoti mbele yake, wote ambao hawawezi kudumisha uhai wao.” (Zaburi 22:27). “Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia” (Zaburi 67:4). Kwa hivyo wakati huduma wa Kristo Yesu ulifika kilele hapa ulimwenguni, alitangaza mpango wake wazi wazi: “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. Toba na msamaha wa dhambi utatangazwa kupitia Jina Lake, kuanzia Yerusalemu” (Luka 24:46-47). “Kwa sababu hii, enedeni ulimwengu mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi” (Mathayo 28:19).

Bwana Yesu Kristo siyo mwokozi tu wa mataifa fulani au makabila fulani. Yeye si wa taifa moja pekee. “Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” (Yohana 1:29). “Kwa maana hakuna tofauti kati ya tofauti kati ya Myahudi na Myunani, Yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao. Kwa maana, ‘Kila mtu atakayeliita Jina la Bwana, ataokoka’ ” (Warumi 10:12-13). Mwite sasa na ungane na watu wake ambao wako katika kila pembe la ulimwengu.