Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kuzivua enzi na mamlaka

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Disarm the Rulers and Authorities

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 42 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Akiisha kuifuta ile hati yenye mashtaka yaliyokuwa yanatukabili
pamoja na amri zake, aliiondoa isiwepo tena, akiigongomea
kwenye msalaba Wake. Mungu akiisha kuzivunja enzi na
mamlaka, alizifanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa
kuziburuza kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba wa
Kristo.” (Wakolosai 2:14-15)

“Mwana wa Mungu alidhihirishwa ili aziangamize kazi za Ibilisi.” (1 Yohana 3:8)

Kuna wakati katika Biblia ambapo mistari kama huu wa enzi na mamlaka humaanisha serikali za ulimwengu huu. Lakini tunaposoma kwamba msalabani Kristo alizivua enzi na mamlaka na kuzifanya mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo, Biblia inazungumza kuhusu nguvu za shetani ambazo hutawala ulimwenguni. Tunaona jambo hili wazi katika Waefeso 6:12 wakati Biblia inasema kwamba, “Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo katika ulimwenguni wa roho.”

Katika Biblia shetani anaitwa “mungu wa dunia” mara tatu. Wakati Kristo alikuwa karibu kufa msalabani, alisema, “Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.” (Yohana 12:31). Kwa kifo cha Bwana Yesu Kristo shetani alishindwa na mapepo wake. Wote walishindwa msalabani.

Jambo hili halimaanishi kwamba wao hawako tena ulimwenguni. Hata sasa tunapigana nao. Lakini tunapigana na maadui ambaye ameshaa shindwa. Sisi tunajua kwamba tuko na ushindi. Ni kama mnyama ambaye kichwa chake kimekatwa na anakimbiakimbia hapa na pale akiwa na ukali mwingi hadi wakati atakapoanguka afe. Vita vimesha shindwa, lakini tunafaa tuwe waangalifu sana kwa sababu shetani bado anaweza kuleta uharibifu.

Wakati Bwana Yesu Kristo alikufa, Mungu alikuwa, “Akiisha kuifuta ile hati yenye mashtaka yaliyokuwa yanatukabili pamoja na amri zake, aliiondoa isiwepo tena, akiigongomea kwenye msalaba Wake.” (Wakolosai 2:14). Hivi ndivyo alivyozivua enzi na mamlaka na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri. Kwa ufupi sheria ya Mungu haituhukumu tena kwa sababu Kristo alilipa fidia ya dhambi zetu. Shetani hawezi tena kutushitaki.

Kabla ya Kristo Yesu kuzifidia dhambi zetu, shetani alikuwa akiwashitaki watu wake. Jina shetani linamaanisha adui au mwenye kutushitaki. Lakini baada ya kifo cha Bwana Yesu Kristo, jambo muhimu lilitendeka. “Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema, ‘Sasa Wokovu na weza na Ufalme wa Mungu wetu umekuja na mamlaka ya Kristo wake. Kwa kuwa ametupa chini mshtaki wa ndugu zetu, anayewashtaki mbele za Mungu usiku na mchana.” (Ufunuo 12:10). Kristo amemshinda mshitaki na amemtupa chini.

Sasa baada ya kuokoka hakuna mashitaka yanaweza kuletwa dhidi yetu. “Ni nani atakayewashtaki wale ambao Mungu amewachagua? Ni Mungu mwenyewe ndiye mwenye kuwahesabia haki.” (Warumi 8:33). Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kuwashitaki wateule wa Mungu. Kristo ndiye haki yetu kwa hivyo mshitaki wetu amevuliwa mamlaka. Hawezi kutushitaki tena, na akifanya hivi ataibishwa. Kwa hivyo watu wa Mungu wako huru kumtumikia Mungu kwa furaha. Hatumtumikii Mungu tukiwa katika utumwa au uoga, tunamtumikia kwa sababu tumewekwa huru ili tuweze kumtumikia.